Lamentations 1:7-10


7 aKatika siku za mateso yake na kutangatanga,
Yerusalemu hukumbuka hazina zote
ambazo zilikuwa zake siku za kale.
Wakati watu wake walipoanguka katika mikono ya adui,
hapakuwepo na yeyote wa kumsaidia.
Watesi wake walimtazama
na kumcheka katika maangamizi yake.

8 bYerusalemu ametenda dhambi sana
kwa hiyo amekuwa najisi.
Wote waliomheshimu wanamdharau,
kwa maana wameuona uchi wake.
Yeye mwenyewe anapiga kite
na kugeukia mbali.

9 cUchafu wake umegandamana na nguo zake;
hakuwaza juu ya maisha yake ya baadaye.
Anguko lake lilikuwa la kushangaza,
hapakuwepo na yeyote wa kumfariji.
“Tazama, Ee Bwana, teso langu,
kwa maana adui ameshinda.”

10 dAdui ametia mikono
juu ya hazina zake zote,
aliona mataifa ya kipagani
wakiingia mahali patakatifu pake,
wale uliowakataza kuingia
kwenye kusanyiko lako.
Copyright information for SwhNEN